John 4:19-26

19 aYule mwanamke akasema, “Bwana, naona bila shaka wewe ni nabii. 20 bBaba zetu waliabudu kwenye mlima huu, lakini ninyi Wayahudi mnasema ni lazima tukaabudu huko Yerusalemu.”

21 cYesu akamjibu, “Mwanamke, niamini, wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala huko Yerusalemu. 22 dNinyi Wasamaria mnaabudu msichokijua. Sisi Wayahudi tunamwabudu Mungu tunayemjua kwa sababu wokovu unatoka kwa Wayahudi. 23 eLakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo halisi, watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu namna hii, ndio Baba anawatafuta. 24 fMungu ni Roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”

25 gYule mwanamke akamwambia, “Ninafahamu kwamba Masiya (aitwaye Kristo) anakuja. Yeye akija, atatueleza mambo yote.”

26 hYesu akamwambia, “Mimi ninayezungumza nawe, ndiye.”

Copyright information for SwhNEN